Saturday, August 11, 2012

Vichwa vitatu vyakimbizana T-Moto

 Jokha Kassim

Mbali na hilo wamekuwa na mashabiki nyomi huku Jokha, akionekana hodari zaidi mara baada ya kuibuka kwenye kundi maarufu la Zanzibar Stars Modern Taarab.
Ni wale nyota watatu wenye uwezo mkubwa wa kuimba muziki wa taarabu hapa nchini, Jokha Kassim, Mwanahawa Ally ‘Chipolopolo’ na Nyawana Fundikira, wameanza kukabana koo, kila mmoja akihitaji umalkia wa bendi ya T-Moto Modern Taarab.
Naye Ofisa Mipango wa bendi hiyo, Kais Mussa Kais, alisema, mnyukano huo kwa waimbaji wao ni sehemu ya mafanikio ya T-Moto.
Ingawa wamesheheni waimbaji wengi, lakini waimbaji hao, Jokha, Nyawana na Mwanahawa, wameonekana kugongana vilivyo katika mazoezi yao.
Alisema hiyo ni pamoja na sehemu ya mafanikio ya bendi yao, kutokana na ushindani kwa waimbaji wao, hivyo wanadhani waachie wenyewe katika hilo kuwania umalkia.
Na imekuwa na waimbaji nyota sehemu mbalimbali duniani, hasa kwa bendi za Tanzania, kitu ambacho mara nyingi huleta tunu, maana mashabiki ndio waamuzi na wanaowaunga mkono.
Waimbaji wengine wa T-Moto ni pamoja na Aisha Masanja, Shimuna Kassim, Amina Rashid, Hanifa Juma, Shaban Ramadhan, Mrisho Rajabu, Rahma Omari, Silver Mwandilee, Kasikile Msukule na wengineo.

No comments:

Post a Comment